HAYA NDIO MAZOEZI YA KUUFANYA UKE KUA MDOGO NA KUBANA..[KEGEL EXERCISE]
Sababu nyingi sana zinaweza kuchangia kupungua kwa nguvu za misuli ya uke na na tumbo la chini kwa ujumla ikiwemo ujauzito, umri mkubwa, kuzaa watoto, upasuaji na kua na uzito mkubwa.
Mazoezi ya kegel husaidia kukaza misuli inayoshikilia viungo vya chini ya tumbo ikiwemo mfuko wa uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo na uke..
Wanawake wengi ambao wana misuli iliyolegea hawafiki kileleni kirahisi wakati wa tendo la ndoa na wakati mwingine huhitaji uume mnene ili kusugua mishipa yao ya fahamu ya uke kirahisi na kufika kileleni kuliko wanaofanya mazoezi haya. Lakini pia mzazoezi haya husaidia kuzuia mkojo kutoka wakati wa kucheka, kushindwa kuzuia mkojo ukibana na kushindwa kuzuia choo kubwa ikebana..
Elimu ya afya ya nchi ambazo hazijaendelea kama Tanzania hujali zaidi kutibu na kuzuia magonjwa ila sio matatizo kama haya..
Hivyo kama mwanamke una tatizo hili au mwenzako ana tatizo hili twende pamoja ili uweze kurudi kwenye maisha yako bora ya zamani ulipokua mbichi..
Jinsi ya kufanya mazoezi haya….
Tafuta msuli sahihi…
Kuufahamu msuli wa kuufanyia mazoezi nenda chooni kukojoa alafu katikati ya kukojoa zuia mkojo. Ukifanikiwa huo ndio msuli sahihi..
Fanya mazoezi sasa….
Baada ya hapo malizia mkojo wako kisha nenda kitandani..lala kwa mgongo kaza msuli uleule uliokaza wakati wa kuzuia mkojo. Kaza msuli kwa sekunde kumi kisha legeza kwa sekunde kumi.
Kua makini….
Kwa matokeo mazuri kaza msuli huo tu, usikaze misuli ya tumbo, mapaja au makalio. Usibane pumzi pumua tu kawaida wakati wa zoezi hili.
Fanya mara tatu kwa siku..
Kaza na kuachia msuli huo mara kumi asubuhi, vivo hivyo mchana na jioni.. lakini pia unaweza kukaza msuli huo popote ulipo ata kama hakuna sehemu ya kulala kwa mgongo. Kwenye foleni ya benki, kwenye gari, ukiwa ofisini kwani hakuna mtu atakayegundua unafanya nini..
Mwisho: mambo yote ninayo ongelea kwenye hii blog yanawezekana tu iwapo mtu ana bidii ya kufanya kitu husika. Usifanye kitu kwa wiki moja ukategemea mabadiliko yeyote. Kila kitu